ismailjussa

Archive for the ‘Public Policy’ Category

Ungana na CUF kupitia Dira ya Mabadiliko

In Public Policy on August 25, 2010 at 9:11 pm

Nini Dira ya Mabadiliko?

Baada ya kuchoshwa na miaka 49 ya utawala wa CCM na watangulizi wake, Watanzania sasa wanataka mabadiliko ya kisiasa. Lakini mabadiliko hayo hayawezi kuja kwa njia za kushtukiza tu. Watanzania wanastahiki kuwa na Dira ya Taifa ya kujenga nchi inayoheshimu haki za binadamu, yenye misingi mizuri ya demokrasia ambapo raia wote watu wazima na wenye akili timamu wana haki ya  kushiriki kikamilifu katika uamuzi wa masuala yanayohusu maisha yao na hatima ya nchi yao.

Ni kwa sababu hiyo, CUF sasa inakuja na Dira ya Mabadiliko (Vision for Change) ambayo inakusudia kuitumia kuongoza harakati za kuing’oa madarakani CCM kupitia Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 31, 2010.

Dira ya Mabadiliko tunayowapelekea watanzania, ambayo ndiyo itakuwa msingi wa ilani ya Uchaguzi wa CUF kwa mwaka huu wa 2010, na ambayo tutawaomba waiunge mkono kupitia uchaguzi Mkuu huu inatilia mkazo mambo 22 ambayo tuaamini chini ya Serikali ya CUF yatatujengea Tanzania Mpya inayojili haki sawa kwa wananchi wote na itakayojenga uchumi imara unaoongeza ajira na utakaoleta neema na tija kwa wote. Mambao hayo 22 ni haya yafuatayo:-

1. Kila raia popote alipo awe na haki ya kuchagua na kuchagukiwa kuwa kiongozi toka ngazi kitongoji/kijiji mtaa mpaka uongozi wa taifa

2. Kujenga umoja wa kitaifa wa kweli ambapo hakutakuwa na ubaguzi wa aina yeyote wa jinsia, kabila, rangi, dini au ulemavu. Kuhakikisha kuwa serikali inaheshimu dini zote na inajenga mazingira ya waumini wa dini mbali mbali kuheshimu na kuvumiliana

3. Kuhakikisha kuwa kila mwananchi ana uwezo au anawezeshwa kupata milo mitatau kwa siku. Hatua za makusudi zichukuliwe kuhakikisha kuwa kinamama wajawazito na watoto wachanga wanapanga lishe bora kwani mtoto mchanga asiye na lishe bora ananyimwa haki na kujenga mwili, kinga ya mwili na ubongo wake ili aweze kushiriki kikamilifu katika kujielimisha na kujiendeleza na kufikia uwezo wake aliojaaliwa na Mwenyezi Mungu.

4. Kuhakikisha kuwa kila raia ana haki na anapata huduma za msingi za afya. Hatua maalum zichukuliwe kuhakikisha kua huduma za uzazi anapatiwa kila mama mjamzito ili kupunguza vifo vingi vya kusikitisha vya kina mama wajawazito

5. Wazee wengi badala ya kulitumikia taifa kwa muda mrefu wanaishi katika umasikini wa kutisha. Watoto wao hawana kipato cha kutosha na maadili ya kuwalea wazee yameporomoka. Kama taifa ni muhimu turejeshe na kujenga maadili ya kuwaheshimu na kuwaenzi wazee wetu. Tuweke utaratib wa kitaifa wa hfidhi ya wazee itakayohusisha jamii kuwalea wazee wetu

6. Watanzania milioni 4.2 sawa na asilimia 10 ya watanzania wote ni watu wenye ulemavu. Watu wenye ulemavu wana mahitaji sawa na watu wengine, akini pia wanakuwa na mahitaji wengine zaidi kulingana na aina ya ulemavu walio nao. Kipimo cha utu wa taifa ni namna kinavyowajali walemavu wake. Serikali itayoongozwa na CUF itatenga fungu maalum la kuwasaidia walemavu wapate elimu, matibabu na vifaa vya kuwapunguzia dhiki ya ulemavu wao na mafunzo stahiki waweze kuajirika na kuajiriwa katika fani mbali mbali

7. Elimu ndio ufunguzi wa maisha. Ili kujenga taifa linalojiamini, watoto wote wa Tanzania wawe na haki ya kupata elimu bora ya msingi, ya sekondari na elimu ya juu. Taifa lijenge utamaduni wa kuamini kuwa elimu haina mwisho na kila raia ajiendeleze kielimu hasa kwa kutumia vizuri teknolojia ya habari na mawasiliano

8. Elimu ya wasichana ni nyenzo muhimu ya kuleta haki sawa kwa wananchi wote na kuhakikisha kizazi kijacho kinakuwa na kufsa sawa katika kuleta na kuneemeka na maendeleo. Wasichana wengi hawamalizi masomo yao kwa sababu ya uwezo mdogo wa fedha wa wazazi, mila zilizopitwa na wakati zinazowabagua wasichana na wanawake, mazingira mabovu ya shule kama vile kutokuwa na vyoo vya wanawake mashuleni na mambo mengine kama hayo. Motisha maalum itolewe kwa wasichana na familia zao ili wasichana wamalize elimu ya shule ya msingi na waendelee na elimu ya sekondari na ya vyuo vikuu na hivyo kuwawezesha kufika uwakilishi wa kujiamini wa 50 kwa 50 wanawake wenye vyombo vya juu vya maamuzi

9. Kuwaelimisha wasichana na wanawake kushiriki katika soko la ajira ni nyenzo muhimu ya kuvunja mduara wa umasikini unaorithisha umaskini toka kizazi kilichopo na kinachofuata

10. Ili kufanikisha mabadiliko ya kiuchumi, kuongeza tija na ajira, Tifa litoe kipaumbele maalum katika kuendeleza elimu ya hisabati, sayansi na teknolojia

11. Kujenga uchumi wa kisasa wenye ushindani kimataifa na utakaohimili misukosuko ya utandawazi, unaokua kwa kasi bila kuharibu mazingira na wenye manufaa kwa wananchi wote kuweka misingi ya utawala bora na utekelezaji wa sera utakaohakikisha kuwa uchumi unakua kwa asilimia 8 – 10 kwa miongo mitatu (miaka 30) ijayo

12. Wananchi wahisi na waone kuwa uchumi wa taifa unatoa fursa sawa kwa wananchi wote. Tofauti za vipato vya wananchi wisiwe vikubwa mno huku tukizingatia kutoa motisha kwa raia kuwa wabunifu na wajasirimali hodari. Mikakati ya kufaidi matunda ya kukua kwa uchumi

13. Bila kukuza uchumi umasikini uliokithiri utakuwa tatizo la kudumu katika suala la kukuza uchumi hakuna miujiza. Uchumi unakua kwa kuongeza elimu, ujuzi na utaalamu wa wafanyakazi, ongezeko la rasilimali na vitendea kazi, na kuongezeka kwa ufanikishaji na tija katika uzalishaji na huduma. Kukua kwa uchumi kunahitaji uongozi imara za utawala bora, mikakati na mipango mizuri ya maendeleo na utekelezaji mzuri wa mikakati na mipango hiyo. Kazi ya kukuza uchumi itakuwa rahisi ikiwa tutatumia rasilimali na maliasili ya nchi hii kwa manufaa ya wote

14. Nchi ambazo zimefanikiwa kukuza uchumi kwa kasi ya juu na kuwa na maendeleo kwa muda mrefu zimefanya hivyo kwa kuwa na uongozi adilifu, wenye dira na ulio imara katika kufanya maamuzi, utekelezaji na kujifunza toka kwenye makosa waliofanya na kujirekebisha. Uongozi wa nchi unawajibika kubuni sera kwa kuzingatia uhalisia na hali ya uchumi wa nchi, fursa zilizopo na vikwazo vinavyoikabili nchi katika kukuza uchumi wake. Baada ya kubuni sera, uongozi unawajibika kuzieleza sera hizo kwa wananchi na kuwahamasisha waziunge mkono na waelewe kuwa ili kujinasua toka dimbwi la umasikini wanawajibika kuchapa kazi kwa bidii, kuweka akiba kuwa wajasirimali wabunifu na kukubali kasi ya mabadiliko itawapo fursa watanzania kupata uongozi adilifu, wenye dira, na ulio imara katika uamuzi na utekelezaji

15. Tunapaswa kukipa kilimo nafasi ya pekee katika mikakati ya kukuza uchumi na hivyo kuwaondolea umasikini wananchi wa vijijini ambao wameumizwa vibaya na sera mbovu za CCM zisizotoa kipaumbele kwa kilimo. Katika miaka mitano ijayo, bajeti ya sekta ya kilimo itamuwa asilimia 10 – 15 ya bajeti yote na italenga katika kuimasisha utafiti na elimu kwa wakulima na huduma za ugani, upatikanaji wa mbolea na pembejeo nyingi kwa bei nafuu, bei nzuri kwa wakulima, msoko ya uhakika, kutengeneza barabara za vijiji, kusambaza umeme vijijini kwa kutumia nishari mbadala kama vile biogas inayotokana na mabaki ya mimea na vinyesi vya mifugo, jua na upepo

16. Ukuaji wa uzalishaji wa mazao ya chakula ndio unaoweza kupunguza kasi ya kuongeza kwa bei za vyakula. Kilimo kitaendelea kuwa chanzo muhimu cha mapato ya fedha za kigeni. Tanzania ina ushindani wa biashara katika soko la dunia siyo tu kwa mazao kama vile kahawa, chai, korosho, katani, tumbaku na karafuu lakini pia katika mazao ya vyakula yakiwemo mahindi, mpunga, alizeti, ufuta, jamii ya kunde, mboga mboga na matunda na mibono inayoweza kutumiwa kutengenezea dizeli mbadala na inalinda mazingira. Sekta ya kilimo ni kiungo muhimu cha kukuza sekta nyingine. Mapato ya wakulima yanatumiwa kununua bidhaa za viwanda na huduma nyengine. Wakulima wenye kipato kikubwa watanunua nguo, vyakula vilivyosindikwa kama vile mafuta ya kupikia, mabati, saruji, samani, magodoro na bidhaa nyingine. Ongezeko la mahitaji ya bidhaa hizi vitaongeza ajira viwandani.

17. Kuna changamoto mpya ambazo zinaongeza vikwazo lakini pia kutoa fursa za kukuza uchumi. Ongezeko la joto duniani limeanza kuongeza ukame, litaongeza maji baharini kutoka thekuji inayoyeyuka katika bara la Afrika na Arctic na kuleta mafuriko katika fukwe za pwani, kuongezeka mafuriko, na milipuko ya maradhi. Nchi masikini ambazo zimechangia kidogo sana katika ongezeko la joto duniani ndizo zitakazo athirika zaidi. Mkakati wa kukuza uchumi uzingatie changamoto ya ongezeko la joto duniani. Ulinzi wa mazingira, upandaji wa mashamba ya miti na utumiaji wa nishati mbadala viwe vyanzo vya wananchi kujipatia kipato

18. Hakuna nchi iliyofankiwa kukuza uchumi kwa kiasi ya juu kwa muda mrefu bila serikali kuwekeza kwa kiasi kikubwa katika miundombinu, barabara, nishati, reli, bandari na mawasiliano. elimu na afya. Uwezekano wa serikali katika sekta ya miundombinu, elimu na afya unajenga msingi imara unaovutia sekta binafsi kuwekeza katika shughuli za uzalishaji na biashara. Uwekezaji wa sekta ya umma katika maeneo hayo unatengeneza njia ya kuwezesha viwanda na makampuni mapya kuanzishwa na kuongeza faida ya shughuli zote za kibiashara zinazofaidika kwa kuwepo wafanyakazi wenye afya njema na walioelimika, kuwepo kwa barabara nzuri zinazopitika wakati wote, na kuwepo kwa umeme wa uhakika. Tutawekeza katika miundombinu kwa kutumia vizuri fedha za umma na kukusanya alau asilimia 20 ya pato la taifa kama mapato ya ndani ya serikali

19. Mapinduzi ya kilimo yatayoongeza uzalishaji na tija ni muhimu katika kuanzisha ukuaji wa uchumi endelevu. Lakini kilimo peke yake hakiwezi kukuza pato la taifa kwa muda mrefu. Kuongezeka kwa tija katika kilimo kutaruhusu nguvu kazi kubwa iweze kuajiriwa katika sekta nyengine hususan viwanda. Sekta ya madini kwa ujumla haitoi ajira kwa wingi. Kwa nchi ndogo kuendelea, hakuna njia nyenginwe bali kujijengea uwezo wa kuzalisha bidha za viwanda na kuziuza nchi za nje. Hakuna nchi iliyoendelea na kukuza uchumi wake kwa muda mrefu bila kuwa na maendeleo ya viwanda. Mabadiliko ya mfumo wa uchumi ni kichocheo cha ukuaji wa uchumi. Nguvu kazi ya nchi inahama toka sekta zenye tija ndogo na kwenda kwenye sekta zenye tija kubwa. Viwanda kwa kawaida vina tija ya juu. Nchi ambazo uchumi wake haukui kwa kasi kubwa zimeshindwa kuhamisha rasilimali ya nguvu kazi kwa wingi zinatioa ajira. Kuongezeka kwa mahitaji ya wafanya kazi viwanda husaidia kuongezeka mishahara. Viwanda vingi vinavyohitaji wafanyakazi wengi hupata fursa wanawake kuajiriwa na hivyo kuchangia katika kuleta usawa wa kijinsia

20. Nchi ambazo hazina maendeleo ya viwanda na zinataka kuanzisha viwanda na kuuza nje bidhaa za viwanda zinakabiliwa na ushindani, siyo tu wa nchi zilizoendelea za Ulaya, Marekani na Japan, kalini ushindani mkubwa ni kutoka nchi nyingine za Asia na hasa China. Bidhaa kutoka china zinashindana na makampuni yanayotengeneza bidhaa za viwandani na kuuza soko la ndani. Je Tanzania tunaweza kumudu ushindani wa china katika kuzalisha bidhaa za viwanda?. Gharama za uzalishaji viwandani china zinapanda kwa sababu uchumi wa china unakua kwa kasi ya juu mno. Tayari china inakabiliwa na migogoro ya wafanyakazi wanaodai kuongezwa mishahara. Serikali ya china inashindikizwa na Jumuia ya kimataifa kuongeza thamani ya sarafu yake na kutegemea zaidi soko la ndani katika kukuza uchumi wake. Ikiwa tutajipanga vuziri tunaweza kupenya katika soko la dunia la bidhaa za viwandani

21. Jambo moja linalokwaza sana maendeleo ya viwandani ni ukosefu wa miundombinu ikiwa ni pamoja na umeme wa uhakika, maji, mawasiliano, barabara, reli, bandari n.k Matumizi ya serikali ikiwa ni pamoja na matumizi yanayofadhiliwa na misaada ya nje yalenge katika kuimarisha na kuboresha miundombinu. Ni muhimu pia kuimarisha utaratibu wa usafirishaji wa bidhaa na matumizi ya TEKNOHAMA kupunguza gharama za kufanya biashara. Tunahitaji pia kuanzisha maeneo maalumu ya viwanda ya kutengenezea biadhaa za kuuza nje na kuyasheheni maeneo haya na huduma za umeme, maji, mawasiliano, barabara n.k. katika hilo, tunapaswa kuchagua eneo maalumu kuzingatia hali halisi ya kuwafanya wawekezaji wa sekta binafsi wavutiwe na maeneo hayo

22. Fedha nyingi za umma zinaibiwa au kutumiwa vibaya. Tathmini na uhakika wa kina wa fedha za msaada wa dola milioni 60 uliotolewa na serikali ya Norway katika wizara ya maliasli na utalii katika lipindi cha miaka 12 uliofanyika mwaka 2006 unaonyesha kuwa nusu ya fedha hizo, yaani dola milioni 30, ziliibiwa au kutumiwa kifisadi. Tatizo la matumizi mabaya ya fedha haliko wizara ya maliasili na utalii tu bali limetapakaa serikalini kote. Tukidhibiti matumizi mabaya ya feha tunaweza kuokoa fedha zitakazotumiwa katika ujenzi wa miundombinu. Rais Kikwete alipokuwa anafungua Mkutano wa TAKUKURU alieleza asilimia 30 ya matumizi yote ya serikali kila mwaka yanaibiwa au kutumiwa kifisadi. Hii ni sawa na shilingi trilioni 11.8 kwa bajeti ya serikali ya mwaka 2006/7- 2010/11, fedha inayotosha kukamilisha mradi ya kufua umeme MW 2000 na kujenga bara bara za lami km 4000 na kuongeza kima cha chini cha mshahara wa watumishi wa serikali.

Mpaka hivi sasa hatuna Dira ya Maendeleo na mikakati madhubuti ya utekelezaji inayoeleweka kwa wananchi wote. Dira ya Maendeleo ya 2025 ilitayarishwa na wataalamu kuliko kuwashirikisha jamii kwa ujumla, haieleweki kwa wananchi wengi na haitumiwi kuhamasisha wananchi katika ujenzi wa taifa letu. Ukosefu wa uongozi ni kizingiti kikubwa kinachozuia kupitia, kuchambua na kubuni dira ya maendeleo inayozingatia hali halisi ya nchi yetu na mabadiliko ya uchumi duniani.

 

DIRA YA MABADILIKO (VISION FOR CHANGE) YA CUF inakusudia kuonyesha njia ya kuleta haki sawa kwa wananchi wote na kujenga uchumi imara unaokua na kuleta neema na tija kwa wananchi wote.

  

Kwa nini CUF kiongoze mabadiliko Tanzania?

  1. Chama Cha Wananchi (CUF) ndiyo chama kikuu cha upinzani hapa Tanzania. CUF kinasimamia kuwepo kwa Serikali inayomjali kila mmoja wetu. CUF kinaamini katika uhuru wa mtu na uwezo wa kujisimamia dhamana zake, kinaamini katika haki za binadamu na amani ya kweli, na kinaamini katika haki na utawala wa sheria. CUF ni chama kinachojali na kinachotaka mabadiliko yatakayotupa mustakbali mwema katika utulivu.
  2. Chama Cha Wananchi (CUF) kikiwa pamoja na familia za Watanzania kinataka kuwepo elimu bure na yenye manufaa hadi sekondari na kutoa mikopo ya asilimia mia moja kwa wanafunzi wa elimu ya juu na pia huduma bure na zinazoridhisha za afya ya msingi kwa wananchi wote. CUF kinafahamu na kuelewa maisha ya wasiwasi ya familia za Watanzania yanayotokana na kupanda mara kwa mara kwa gharama za maisha, upungufu wa chakula na maji safi na salama, ukosefu wa ajira na usalama wa ajira zilizopo na pia kushindwa kwa Serikali iliyopo madarakani kutekeleza ahadi zake ilizozitoa.
  3. CUF ina sera imara na zenye ufanisi zitakazotujengea uchumi wa kisasa na wenye tija na neema unaotilia mkazo ukuzaji na uimarishaji wa kilimo na kutoa ajira nyingi na bora, wenye kuhakikisha soko za bidhaa za wakulima na kuongeza pato la familia. CUF inawaunga mkono Watanzania wote katika mapambano yao ya kuleta maisha bora na yenye heshima kwa utu wa binadamu.
  4. CUF ni Chama Mbadala kilichodhamiria kuongoza Serikali Mbadala itakayojenga Tanzania mpya isiyo na woga, ukandamizaji, ufisadi, uvunjwaji wa haki za binadamu na vitisho. CUF iko pamoja na wananchi wote wanaoathirika kutokana na kushindwa kabisa kwa serikali isiyo na uwezo na ya kifisadi, na inatoa matumaini mapya kwa wote wanaokandamizwa, kuonewa na kukatishwa tamaa na watawala waliopo.
  5. Wananchi wa Tanzania kwa ujumla wao, bila ya kujali dini, kabila, rangi, tabaka au jinsia zao, wanaweza kuiamini CUF na viongozi wake wa ngazi mbali mbali. Wananchi wote wanaotaka kuleta mabadiliko kwa ajili ya mustakbali mwema wenye kutoa neema, amani, haki na uadilifu wanapaswa kuiunga mkono CUF kwa kujiunga nacho kuleta mabadiliko hayo kuanzia mwaka huu 2009 na kuikamilisha 2010. Sisi tuko tayari.

 ZINDUKA MTANZANIA UUNGANE NA CUF KULETA MABADILIKO

TANZANIA BILA CCM INAWEZEKANA.

 

Advertisements

Seif: My vision for a new Zanzibar

In Public Policy on August 5, 2010 at 6:37 pm

 

 

by Seif Sharif Hamad

Published in Vodaworld magazine

 

On June 27, I was endorsed by the delegates to the National Conference of the Civic United Front (CUF) with a resounding 98 per cent votes to be the party’s flag bearer in this year’s Zanzibar presidential election.

I look forward to participating in this election which I believe will be different from all the elections that have been held since our country re-introduced multi-party system 18 years ago.

I believe this year’s election will be one of peace and hope. The new political rapprochement that has ushered into reconciliation (Maridhiano) that I and President Amani Karume initiated last year and that President Jakaya Kikwete has supported courageously has created an unprecedented opportunity to create a government of national unity in Zanzibar.

CUF has always supported the idea of a government of national unity as it realizes that without the unity of the major elements that form the Zanzibari society there will be no peace to concentrate on important issues of meaningful and sustainable development. I am prepared to work with the CCM candidate in a government of national unity to build a new Zanzibar. I believe the same spirit of dialogue and mutual respect that has led us to internal reconciliation in Zanzibar can be employed to make our Union much stronger and viable for the benefit of the people from both sides of the Republic.

But what is my vision for Zanzibar?

My vision for a future Zanzibar is one where there is unity , yet people will have their own poltical convictions and feel free to express themselves. We will have unity in diversity; everyone will be proud to be a Zanzibari, regardless of his or her ethnic backround or religion. We must heal the scars of history by not allowing any discrimination and by ensuring equal rights and opportunities for all. All of us should promote the idea that all Zanzibaris are united by a common history and destiny. We need a harmonious and tolerant society, in which democracy and mutual respect are well established.

My vision is also to see Zanzibar returning to its rightful position as a tolerant and open society, and a permanent centre of teaching and learning in East and Central Africa. This will have to mean a much greater investment in education, both knowledge and ethical/character education, as a way to construct a knowledge and ethical society that will at once and the same time attract international missions, trade and investments, and employment as an antidote to the politics of hatred and divisions that engulfed our islands for over 50 years.

Our next serious challenge is the economy – how to make a living for our people? I want to see a Zanzibar that is economically developed, where all have employment and can afford the essential of life. CUF is a liberal party and we believe socially inclusive free market policies will serve well a natural entrepreneurial society that Zanzibar is and has always been.

Ours is essentially an agricultural society and relies heavily on the export of cloves, a monoculture which is very vulnerable to price fluctuations. CUF intends to privatize the clove industry and encourage the local production of food especially those items that can be grown locally. There is an obvious need to modernize our agricultural sector and not to rely on rainfall alone for cultivation especially when it comes to food security, an essential component of any autonomous society.

After modernizing the not too productive backbone of our society, i.e. agriculture, I would like to see the government invest heavily in the twin and related areas of education and development. We consider trade, tourism and manufacturing as the three vital sectors that can create new wealth for the new Zanzibar.

Zanzibar was the most prosperous trading centre in East Africa. CUF supports free international trade and foreign investment. We would like to build a free trade zone in Zanzibar. We also need to encourage sustainable use of marine resources. Our people are entrepreneurial and will prosper if we enable free trade without corruption.

If I will be elected, government of national unity that I will lead would be ready to invest resources in intellectual pursuits and human resources development to ensure high quality of intellectual and professional recruitment and retention of staff in relevant institutions. The greatest wealth of Zanzibar is its diaspora of highly educated and skilled Zanzibaris who are serving different societies on the globe except their own. A new Zanzibar under government of national unity will naturally welcome home our brothers and sisters who have lived in exile and encourage them to contribute to our society.

We will work very closely with forward looking international organizations such as the World Bank, the UN local entrepreneurship initiative, the WHO malaria eradication project, and the United Nations Development Program to initiate a Zanzibar Human Development Report which we will use as our human development guide in planning our ministries for sustainable development.

A strong and vibrant economy that we intend to build should help us to see well equipped hospitals, clean and safe water for everyone, electricity in every household, reliable and cheap communications, and a road network that is passable all year round.

But our new economic policy will not succeed without the key of cultural change that will deliver positive results in the area of work ethics and winning back the primary allegiance of our employees. Special programme must be designed and implemented to make our civil servants models when it comes to professionalism, accountability, discipline and result-oriented work ethics.

This is my vision and mission for a new Zanzibar.