ismailjussa

Lipumba amtaka Kikwete kwenye Mdahalo

In Uncategorized on July 14, 2010 at 3:45 pm

 

 

Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CUF, Prof. Ibrahim Lipumba amempa changamoto mgombea mwenzake kwa tiketi ya CCM, Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete, akimtaka akubali kushiriki kwenye midahalo mitatu ili kuwapa fursa Watanzania wajue nini mitazamo yao kuhusiana na masuala mbali mbali yanayogusa maisha yao na hivyo kuwapa nafasi ya kuchagua Rais anayewafaa kwa kipindi cha miaka mitano ijayo.

Hayo yamo kwenye barua ya Prof. Lipumba kwa Rais Kikwete ya tarehe 12/07/2010 yenye Kumbukumbu Nam. CUF/DSM/IKL/001/2010. Hapa chini ni barua hiyo kwa ukamilifu:

 

Mhe. Dr.  Jakaya Mrisho Kikwete

IKULU

Dar es Salaam

 

Yah: PONGEZI KWA KUCHAGULIWA KUWA MGOMBEA URAIS KWA TIKETI YA CCM 2010

 

Kwa niaba ya Baraza Kuu la Uongozi la Chama Taifa (CUF – Chama Cha Wananchi) na kwa niaba yangu binafsi nakuandikia barua hii kukupongeza kwa dhati kuchaguliwa kwa mara ya pili na Mkutano Mkuu wa Chama chako kuwa Mgombea wa Urais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya CCM.

Kwa kuwa na mimi nimechaguliwa na Mkutano Mkuu wa Chama changu cha CUF kuwa Mgombea Urais na Vision for Change – Dira ya Mabadiliko inayowataka Watanzania wazinduke. Hivyo kampeni zetu zitajikita katika ujenzi wa hoja kwa Watanzania waweze kujua, wadai na wapate Haki Sawa kwa Wote na raslimali na mali ya asili ya Tanzania itumiwe kwa uadilifu ili ikuze uchumi unaoongeza ajira kwa wingi na kuutokomeza umaskini.

Katika kuhakikisha tunajenga utamaduni mzuri wa demokrasia katika nchi yetu itakayowapa fursa wagombea wa Urais kuwaeleza Watanzania sera na mikakati watakayoisimamia watakapopewa ridhaa ya wananchi kuiongoza nchi, napendekeza tuwe na midahalo mitatu. Midahalo hiyo ijadili maeneo matatu makubwa:-

  • Sera na mikakati ya kukuza uchumi na kuutokomeza umaskini na kuboresha huduma za jamii
  • Utawala bora na ujenzi wa maadili mema ya taifa
  • Mahusiano ya nchi za nje, na Ulinzi na Usalama wa nchi yetu 

Haya ni mapendekezo ya awali. Ili kufanikisha midahalo hii, ni vyema vyama vya waandishi wa habari, Jumuia za dini, wasomi na watafiti na asasi nyingine zisizo za kiserikali zipewe jukumu la kuratibu na kuandaa midahalo. Timu zetu za kampeni zaweza kukutana na kukubaliana asasi au watu watakaoandaa midahalo hiyo.

Pamoja na kuwapa wapiga kura fursa ya kuwapima wagombea wa Urais, midahalo hii itajenga mahusiano mema baina ya vyama na wagombea na kukomaza demokrasia nchini. Ni matumaini yangu utaafiki pendekezo la midahalo ya kampeni na kulipa suala hili kipaumbele ili maandalizi yafanyike mapema.

Hongera sana kwa kuteuliwa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM.

 

HAKI SAWA KWA WOTE.

 

Prof. Ibrahim Haruna Lipumba

 

Advertisements
  1. […] candidate and CUF’s nominee for the presidency, Professor Ibrahim Lipumba, challenges President Jakaya Kikwete (CCM) to a presidential debate as the general election campaign officially […]

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

Connecting to %s

%d bloggers like this: